HOTUBA
YA MKE WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
MHESHIMIWA
MAMA
SALMA KIKWETE
AKIZINDUA
MRADI WA MAFUNZO KWA SEKTA YA GESI NA MAFUTA YA PETROLI
CHUO
CHA MAFUNZO NA ELIMU YA UFUNDI STADI, LINDI,
10
OKTOBA, 2013
HOTUBA YA MKE WA RAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA MAMA SALMA KIKWETE, AKIZINDUA MRADI WA MAFUNZO
YA GESI NA MAFUTA YA PETROLI, CHUO CHA MAFUNZO NA ELIMU YA UFUNDI STADI, LINDI
Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi -
Mheshimiwa Philipo Mulugo (Mb)
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi -
Mheshimiwa
Ludovick Mwananzila
Mkuu
wa wilaya ya Lindi;
Mkurugenzi
Mkuu VETA – Eng Zebadiah S. Moshi
Mkurugenzi
wa Elimu na Mafunzo ya ufundi – Leah Lukindo
Meneja
wa Tanzania wa British Gas – Kate Sullam
Mkurugenzi
wa Tanzania wa Volunteer Service Organisation – Jean Van Wetter
Mkurugenzi
wa VETA kanda ya kusini mashariki – Wilhard Soko
Wakuu
wa vyuo vya VETA Lindi na Lindi
Washirika
wengine wa Maendeleo;
Waheshimiwa
Viongozi wa Vyama vya Siasa;
Waheshimiwa
Wabunge;
Viongozi
wa Serikali;
Viongozi
wa Dini;
Waalimu;
Wageni
Waalikwa;
Wanafunzi;
Mabibi
na Mabwana:
Ndugu Wananchi:
Awali
ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha mahali hapa katika
kutekeleza majukumu ya Kitaifa kwa jamii na hasa vijana ambao ndio kundi lengwa
kwa siku ya leo.
Ninayo
furaha kubwa pia kuja hapa Lindi kuzindua awamu ya pili ya Mradi wa Mafunzo na
Elimu ya Ufundi Stadi kwa ajili ya Sekta ya Gesi na Mafuta ya Petroli wenye
madhumuni ya kuimarisha ajira kwa vijana kupitia ufundi stadi Lindi (Enhancing Employability through Vocational
Training – EEVT).
Ninapenda
kuanza kwa kutoa shukurani na pongezi zangu za dhati na kipekee kwa Kampuni ya
British Gas ya Uingereza, Voluntary Services Organisation (VSO Tanzania) ya
Uingereza, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, VETA, na wote walioshiriki kufanikisha
kuanzishwa na kuendelezwa kwa Mradi huu. Ninapenda
pia, kuwashukuru washirika wengine wa maendeleo ambao wameshiriki kwa namna
moja au nyingine katika kufanikisha kuanza kwa Mradi huu hususan Serikali ya
Uingereza kupitia Idara yake ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID), British Council,
Serikali na wananchi wa Mkoa wa Lindi .
Naipongeza
pia Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi chini ya Mwenyekiti wake Prof. Idrissa Bilal Mshoro pamoja
na Menejimenti ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
inayoongozwa na Eng. Zebadiah Moshi, kwa kuhamasisha uanzishwaji wa Mradi huu
na sasa tuko katika hatua ya pili ya uzinduzi wa mradi kwa mkoa wa Lindi,
hongereni sana. Nina imani kubwa kuwa wataendelea kufanya kazi nzuri ili
malengo ya Mradi huu yaweze kutimia. Pia, ninatambua kazi kubwa iliyofanywa
katika awamu ya kwanza ya mradi huu katika chuo cha ufundi VETA Mtwara na sasa
awamu ya pili kwa VETA Lindi.
Shukurani
za pekee pia ziwaendee kampuni ya British Gas ambayo imeonesha ushiriki mzuri
katika kufadahili mradi huu kwa chuo hiki cha Lindi . British Gas ambao ni
washirika wakuu wa mradi huu Pamoja na mchango mkubwa wa ajira kwa washiriki,
makampuni ya Petroli na Gesi watapata wafanyakazi walioiva vizuri na hivyo
kuongeza tija katika kazi na uzalishaji kwa vijana na jamii ya Lindi na maeneo
ya jirani.
Ndugu Wananchi;
Natambua
kuwa mradi kama huu tayari umeanza kwa mkoa wa Mtwara katika chuo cha ufundi
VETA Mtwara ambapo Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Gharib Bilal
alizindua mradi huo pale Mtwara mwishoni mwa mwaka jana 2012. Ninajisikia
mwenye furaha kufanya vivyo hivyo katika uzinduzi huu kwa mkoa wa Lindi
nikiamini vijana wa Lindi na maeneo mengine watafaidika na fursa hii. Serikali
itaendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wote wa maendeleo kupitia vyombo husika
kama VETA ili kujenga mazingira mazuri ya kutoa ajira.
Nimepewa
taarifa kuwa mradi huu ambao utakuwa wa miaka 2 kuanzia 2013 hadi 2015 ambapo wanafunzi zaidi ya 224 watapata mafunzo
toka kwa walimu wenye uzoefu wa kimataifa kwa kushirikiana na walimu wa hapa
Lindi na kukifanya chuo cha ufundi stadi Lindi kuwa cha kiwango cha kimataifa.
Pia mradi huu utaboresha kozi za chuo
ili ziendane na mahitaji ya soko hususani sekta ya Gesi na Mafuta.
Katika
kufanikisha hilo, nimeambiwa kuwa walimu 4 katika karakana 4 za hapa Lindi
watajengewa uwezo kwa kupewa kozi zenye hadhi ya kimataifa ili wapate tuzo
zinazotambulika kimataifa. Nimefurahi
sana kusikia kuwa walimu hawa 4 tayari wameanza kujengewa uwezo kwa
kushirikiana na wenzao wa VETA Mtwara. Vilevile, Wataalamu wa kimataifa kutoka
shirika la VSO wameanza kutoa ushauri na uzoefu wao kwa kushirikiana na walimu
wetu wa hapa VETA Lindi hasa kwa kuzingitia fursa za gesi na mafuta. Mradi huu
pia utaboresha matumizi ya lugha ya kiingereza kwa walimu wasiopungua 15 kwa
sababu vijana wetu wanatarajiwa kuajiriwa katika makampuni ya ndani na ya
kimataifa, hivyo lugha ya kiingereza nyenzo muhimu ya mawasiliano.
Ndugu Wananchi
Ushiriki
wa wananchi, utayari wao wa kumiliki maendeleo yao na kujituma kwao pamoja na
uongozi na usimamizi mzuri wa Serikali ya Mkoa utakuwa ndio chachu ya mafanikio
ya Mradi huu. Mradi huu utakuwa na mchango mkubwa kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi
, Mikoa ya jirani na Taifa kwa ujumla katika kuboresha hali ya maisha ya kaya kwa
kuwapatia ujuzi mbalimbali katika Sekta ya Gesi na Mafuta ya Petroli, utakao wawezesha
wahitimu kujiajiri au kuajiriwa.
Ndugu Mabibi na Mabwana
Ninatoa
ombi na rai kuwa makampuni mengi yajitokeze kushiriki katika mradi huu kwani
una mafanikio makubwa si kwa wahitimu peke yake bali kwa makampuni pia kwani
watapata wafanyakazi mahiri watakao tumia muda mfupi kuelewa wajibu wao. Wito wangu kwa VETA ni kupanua wigo wa
mashirikiano na waajiri ili tuweze kujenga nguvu kazi itakayokidhi matakwa ya
soko la ajira ili tuweze kufanikiwa kufikia malengo ya mipango ya kitaifa kama
Mpango wa Taifa wa miaka 5, Mkakati wa kukuuza uchumi na kupunguza umasikini
awamu ya 2, Matokeo makubwa sasa (Big Result Now) na hivyo kuifikia dira ya maendeleo
ya Taifa 2025 ya kuwa nchi yenye pato la kati.
Mafunzo ya ufundi Stadi katika nchi mbalimbali imekuwa chachu ya
maendeleo. Ninaahidi kuwa serikali kama
inavyoyapa msisitizo mafunzo ya ufundi stadi kipaumbele, itaendelea kuijengea VETA
uwezo ili iweze kumudu majukumu yake.
Ndugu wananchi
Kwa
namna ya kipekee sana naomba nitoe msisitizo nikiwa kama mama lakini pia kama
mmoja wa wana-maendeleo katika Mkoa wa Lindi. Ninatambua changamoto za mtoto wa
kike katika kupata elimu kwa ngazi zote. Ni matumaini yangu kuwa fursa hii ya
mradi huu itatoa mwanga kwa mtoto wa kike. Nitoe wito kwa wazazi na walezi
kuwajengea mazingira mazuri watoto wa kike ili washiriki sawa na watoto wa
kiume katika kunufaika na mradi huu. Wataalamu wanasema; ukimuelimisha mtoto wa
kike umeelimisha jamii nzima. Tutumie fursa hii vizuri ili vijana wetu wapate
ujuzi wenye viwango vya kimataifa na hivyo kushindana katika soko la ajira la
sasa.
Ndugu wananchi
Nafurahi
kuzindua Mradi huu nikiwa na matumaini makubwa kwamba Watanzania hasa vijana sasa
tumepata moja ya ufumbuzi wa changamoto ya ajira hasa kwa vijana, kwa kutumia
fursa ambazo zimejitokeza katika Sekta hii.
Ndugu wananchi na Wageni Waalikwa,
Baada
ya kusema haya machache, sasa natangaza rasmi kuwa nimezindua rasmi Mradi huu
wa Mafunzo na Elimu ya Ufundi Stadi kwa Sekta ya Gesi na Mafuta ya Petroli kwa
chuo cha ufundi stadi Lindi.
Ahsanteni
sana kwa kunisikiliza.